Home Uncategorized WALTER BWALYA : NIPO TAYARI KUSAINI SIMBA

WALTER BWALYA : NIPO TAYARI KUSAINI SIMBA


WALTER Bwalya mshambuliaji wa Nkana FC ya Zambia amesema kuwa yupo tayari kusaini Simba iwapo watamhtaji.

Bwalya amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba na kuna taarifa kwamba amewaaga wachezaji wenzake kwamba anakuja Bongo kujiunga na Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.

“Sijafanya mazungumzo na Simba mpaka sasa na sijui kama wao wanahitaji huduma yangu, natambua kwamba Simba ni timu kubwa lakini hakuna dili yoyote kati yetu.

“Mkataba wangu wa miaka miwili ndani ya Nkana FC unaelekea ukingoni na nimebakiwa na miezi sita, sheria inatoa nafasi ya mimi kuzungumza na timu yoyote kama itatokea watakuja nitasikiliza ofa yao,” amesema.

SOMA NA HII  HICHI NDICHO KILICHOWAFELISHA SENEGAL AFCON 2019