Home Uncategorized YANGA KUJICHIMBIA MOROGORO MAANDALIZI YA LIGI

YANGA KUJICHIMBIA MOROGORO MAANDALIZI YA LIGI


MABINGWA wa kihistoria wa Tanzania Bara, Yanga leo wametimkia Morogoro kwa ajili ya kuweka kambi.


Msimu wa mwaka 2019-20 unatarajiwa kuanza Agosti 23 na mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya Simba na JKT Tanzania uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa wamechagua Morogoro kutokana na utulivu.

“Timu leo imeelekea Mrogoro kwa ajili ya kambi na itakuwa huko mpaka msimu utakapoanza, tumejipanga kufanya vema msimu ujao ndio maana tunakwenda kuweka kambi sehemu tulivu,” amesema.
SOMA NA HII  MASHABIKI SIMBA WAMUANGUKIA KIBU