Home Uncategorized HAJI MANARA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA NDANI YA SIMBA

HAJI MANARA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA NDANI YA SIMBA

IMEELEZWA kuwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa anampango wa kuachia ngazi ya uongozi ndani ya Simba.

Kwa sasa nafasi ya Ofisa Habari ni miongoni mwa zile ambazo zinatafuta wafanyakazi baada ya Simba kutangaza nafasi za kazi ila bado anashikilia Manara ambaye ndiye Ofisa Habari.

Habari zinaeleza kuwa Manara amesema sababu kubwa itakayomfanya aachie madaraka ndani ya Simba ni pale mashabiki wa Yanga watakapojaza uwanja wa Taifa siku ya Mwananchi Agosti 4 zaidi ya Simba Day Agosti 6.

SOMA NA HII  KAZE AINGIA KWENYE MTEGO MWINGINE NDANI YA YANGA