Home Uncategorized HALI YA MLINDA MLANGO NAMBA MOJA WA LIVERPOOL BADO KIZUNGUMKUTI

HALI YA MLINDA MLANGO NAMBA MOJA WA LIVERPOOL BADO KIZUNGUMKUTI


JURGEN Klopp, Meneja wa Liverpool amesema kuwa hali ya mlinda mlango Alisson inamtia hofu baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Norwich City iliyopanda daraja msimu huu.

Kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England, Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Alisson alishikwa na maumivu ya mguu, zikiwa zimebaki dakika nane kabla ya mchezo kukamilika.

“Kwa kweli hali ya Alisson inatia wasiwasi kwa sasa kwani aliskia kama amepigwa na kitu mguuni hivyo ni jambo la kusubiri kwa sasa,” amesema.

Kipa huyo ni chaguo la kwanza kwani msimu uliopita kwenye jumla ya mechi 21 hakuruhusu bao.

SOMA NA HII  NDANDA: TUPO TAYARI KUVAANA NA SIMBA