Home Uncategorized HIVI NDIVYO SIBOMANA ALIVYOMPA ZAHERA KIBURI

HIVI NDIVYO SIBOMANA ALIVYOMPA ZAHERA KIBURI


KOCHA wa Yanga Mwinyi Zahera, ameanza jeuri kwa kutamka kuwa kwa safu bora ya ushambuliaji aliyonayo hivi sasa hakuna mabeki watakaowazuia kufunga mabao.

Kauli hiyo aliitoa akiwa kambini mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, jana ilicheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika mkoani humo.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inaongozwa na Juma Balinya, Patrick Sibomana, David Falcao Molinga, Sadney Urikhob, Mrisho Ngassa, Maybin Kalengo na Issa Bigirimana.

Zahera alisema ana imani kubwa na safu yake ya ushambuliaji ambayo ndani ya dakika 90 ina uhakika wa kufunga bao.

Zahera alisema kuwa jeuri anaipata kutokana na soka la pasi za haraka wakati wakiwa na mpira wanapofika katikati ya uwanja wakilishambulia goli la wapinzani wao.

Aliongeza kuwa, hivi sasa anachokifanya ni kutengeneza muunganiko mzuri wa washambuliaji watakaocheza kwa kuelewana wanapofika kwenye goli la wapinzani wao.

“Kati ya sehemu ambayo sina hofu nayo, basi safu ya ushambuliaji ambayo muda wowote nina uhakika wa kupata bao kutokana na ubora, uwezo na kasi waliyokuwa nayo pale tunaposhambulia goli la wapinzani wetu.

“Nilichokibakisha ni kitu kidogo cha kiufundi ambacho kabla ya kurudiana na wapinzani wetu Rollers ninataka kiwe kimekamilika nacho ni kutengeneza muunganiko mzuri kama unavyofahamu hichi kikosi ni kipya ambacho nusu ya wachezaji ni wapya na ndiyo sababu ya kuomba viongozi kucheza michezo miwili ya kirafiki.

“Kikubwa ninataka kuona washambuliaji wangu wanaendelea na kasi hiyo nzuri ambayo msimu uliopita haikuwepo kutokana na aina ya wachezaji niliokuwa nao hivi sasa baada ya usajili mzuri nilioufanya,” alisema Zahera.

Yanga inatarajiwa kucheza mchezo huo wa marudiano wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers utakaopigwa Agosti 24, mwaka huu huko Gaborone, Botswana

SOMA NA HII  MANULA AVUNJA UKIMYA, AFTOA TAMKO KUHUSIANA NA KAKOLANYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here