Home Uncategorized KIMENUKA MADRID, ZIDANE NA RAIS WAKE HAKUNA MAELEWANO, NYOTA EPL ATAJWA

KIMENUKA MADRID, ZIDANE NA RAIS WAKE HAKUNA MAELEWANO, NYOTA EPL ATAJWA


Kitendo cha Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez kushindwa kukamilisha harakati za kumsajili kiungo Mfaransa anayekipiga kunako Manchester United, Paul Pogba kimeanza kuleta sintofahamu baina yake na Kocha Zinedine Zidane.

Taarifa zimeripoti kuwa Zidane amekuwa akilitaka jina la mchezaji huyo kwa udi na uvumba ili kuirejesha Real Madrid katika makali yake yake ya mwanzo.

Licha ya uhitaji wake wa kumpata Pogba, bado Perez ameonekana kutia ngumu juu ya kutoa fedha za kumsajili kitu ambacho Zidane hakifurahii.

Hivi karibuni pia Zidane alisema angependa kumuona mchezaji Kylian Mbappe wa PSG akitua Santiago Bernabeu lakini kumekuwa hakuna jitihada zozote za kufanikisha usajili wa straika huyo mwenye mbio za aina zake.

Inaelezwa kuwa maelewano baina ya Zidane na Rais Perez huenda yakafikia pabaya zaidi juu ya mipango ya usajili ambapo mpaka sasa inaonesha kocha huyo hajaridhishwa na usajili uliofanyika.

SOMA NA HII  NIYONZIMA WA YANGA ATIBUA DILI LA KIUNGO HUYU KUTUA YANGA JUMLAJUMLA