Home Uncategorized SADIO MANE NI ANA BALAA NDANI YA LIVERPOOL

SADIO MANE NI ANA BALAA NDANI YA LIVERPOOL


SADIO Mane, mshambuliaji wa kikosi cha Liverpool amesema kuwa furaha yake ni kuona timu yake inashinda kwenye michezo wanayocheza kwa sasa kutokana na ushindani uliopo ndani ya Ligi Kuu England.

Mane leo ameiongoza timu yake ya Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sounthampton kwa kufunga moja ya bao maridadi akiwa ndani ya mstari wa 18.

“Furaha yetu ni kuona timu inashinda na kupata matokeo kwani ndiyo furaha yetu na mashabiki, kwa sasa bado kazi inaanza na mwendelezo mwingine unafuata,” amesema.

Bao la pili lilifungwa na Robert Firmino dakika ya 71 akiwa katikati ya msitu wa mabeki na lile la kufutia machozi kwa wapinzani likifungwa na Danny Ings dakika ya 83 kutokana makosa ya kizembe yaliyoanzia kwa beki na mlinda mlango wa Livelpool.

SOMA NA HII  YANGA: TUNAUTAKA UBINGWA WA LIGI KUU BARA