Home Uncategorized SIBOMANA WA YANGA ATAJA KILICHOMFANYA AKOSE PENALTI JANA KIMATAIFA

SIBOMANA WA YANGA ATAJA KILICHOMFANYA AKOSE PENALTI JANA KIMATAIFA


PATRICK Sibomana, mshambuliaji wa Yanga raia wa Rwanda amesema kuwa kilichomponza ashindwe kufunga penalti jana mbele ya Township Rollers ni hofu aliyokuwa nayo mwanzo kabla ya kupiga mpira huo wa adhabu.

Yanga jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa uwanja wa Taifa kabla ya kupachika bao la kusawazisha dakika ya 86 kwa mkwaju wa penalti.

“Mchezo ulikuwa mgumu na nilikosa penalti kutokana na hofu ambayo nilikuwa nayo, kazi kubwa ambayo tumeifanya tunatambua kuwa inaendelea hivyo tunahitaji sapoti ya mashabiki,” amesema.

Yanga itarudiana na Rolers kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.

SOMA NA HII  SIMBA YATUA KWA STARAIKA HUYU MKONGO