Home Uncategorized YANGA: EVERTON WALIKAA KWA KARIOBANGI HIVYO MECHI ITAKUWA NGUMU, MASHABIKI WAJITOKEZE

YANGA: EVERTON WALIKAA KWA KARIOBANGI HIVYO MECHI ITAKUWA NGUMU, MASHABIKI WAJITOKEZE


DISMAS Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa Agosti 4 haitakuwa nyepesi kwani wanacheza na timu ngumu na watatambulisha pia wachezaji.

Ten amesema:- “Uwanja wa Taifa itakuwa ni kilele cha siku ya Mwanachi ambapo tutacheza na timu kubwa na yenye uwezo mkubwa ambayo ni Kariobangi Sharks kutoka Kenya.

“Hawa ni mabingwa wa SportPesa Super Cup na hivi karibuni imewafunga Everton hivyo si klabu ya kuwabeza na utakuwa ni mchezo mzuri.

“Agosti 4 timu yetu itatambulisha wachezaji wake wote pamoja na jezi, tunawaomba wanachama wote wanunue vifaa halisi ambavyo vinatengenezwa na mzabuni aliyeshinda tenda,” amesema.

Everton ilipomenyana na Kariobangi kwenye mchezo wa kirafiki dakika 90 walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na kupelekea kupigwa penalti ambapo Kariobangi ilishinda penalti 4-3

SOMA NA HII  DAVID KISSU: BADO TUPO IMARA, TUTAREJEA KWENYE UBORA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here