Home Uncategorized AJIBU AINGIA KATIKA ANGA ZA MBELGIJI SIMBA

AJIBU AINGIA KATIKA ANGA ZA MBELGIJI SIMBA


KOCHA wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems juzi kwa mara ya kwanza alianza kazi ya kukinoa kikosi chake na kuonekana akikazia zaidi mazoezi ya fiziki ili kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa fiti.

Aussems alikuwa mapumzikoni kwa muda na hakuwa sehemu ya benchi la ufundi lililosimamia mazoezi ya kikosi hicho juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar lakini jana ameanza kazi rasmi.

Simba kwa sasa wanajiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ukiwa ni wa Ligi Kuu Bara ambao utapigwa Septemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Baadhi ya mastaa ambao walikuwepo mazoezini jana ni Aishi Manula, Ibrahim Ajibu, Pascal Wawa, Mzamiru Yassin, Sharaf Shiboub (Sudan), Wabrazil Gerson Fraga, Tairone Santos na Wilker Henrique.

Baada ya kufika mazoezini saa 4 asubuhi moja kwa moja wachezaji wote walianza program ya mazoezi ya viungo mbalimbali ambapo yalikuwa yakiongozwa na Kocha wa Viungo, Adel Zrane ambaye alionekana kuwakomalia kweli kweli wachezaji ili kuhakikisha wanakuwa fiti.

Walipomaliza program hiyo, wakahamishwa kwenye mazoezi ya uwanjani kwa kuchezea mpira ambapo hapo sasa wakaungana na Aussems ambaye aliwagawanya wachezaji wake katika makundi mawili na kucheza mchezo wa kukabana.

Baada ya kuona sasa wameanza kukaa sawa kimwili, Aussems aliwagawa wachezaji wake katika vikosi viwili na kuanza kucheza mechi kwa muda mfupi kwa kuwa mastaa wake wengi hawapo kikosini humo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kitaifa.

Mara baada ya mazoezi hayo kumalizika, Aussems alizungumza na Championi Jumamosi, ambapo alisema kwa sasa ni ngumu kuwa na program kutokana na wachezaji wake wengi kuwa kwenye majukumu ya mataifa yao.

Aliongeza kuwa hadi kufikia Jumatano ijayo wachezaji wote watakuwa wamerejea hivyo itakuwa rahisi wao kuweza kufanya program za pamoja bila tatizo.

“Tumeanza mazoezi lakini nakosa wachezaji kama 11 wana majukumu mengi ila nimepanga katika mazoezi yangu ya Jumatano itachezwa mechi ila sijui mpaka sasa tacheza na timu gani lakini lengo ni kuwaweka sawa wachezaji wangu.

“Leo tumefanya mazoezi ya viungo na hii yote nataka wawe imara japokuwa tumechezea mpira lakini nina amini kuwa wakirudi wote programu zitakuwa zinaenda sawa. Pia tunatarajia John Bocco ambaye ni majeruhi atajiunga na sisi kuanzia wiki ijayo,” alisema Aussems.

SOMA NA HII  HAWA NDIO MASTAA HATARI DABI YA KARIAKOO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here