Home Uncategorized MESSI AIVURUGA BARCELONA, TETESI ZA SOKA LEO ULAYA JUMANNE HZIKO HAPA

MESSI AIVURUGA BARCELONA, TETESI ZA SOKA LEO ULAYA JUMANNE HZIKO HAPA


Ujumbe mfupi kutoka kwa Lionel Messi huenda ulivuruga mpango wa Barcelona kumsajili tena mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, kutoka klabu ya Paris St-Germain. (L’Equipe, via Star)

Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi angelifanikiwa kumpata Neymar msimu huu ikiwa dau la kuvunja rekodi la euro milioni 300 sawa (£272m) lingemfikia. (Le Parisien, via Sport)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, yuko radhi kuhamia Manchester United baada kukiri kuwa “angelipendelea” kurejea England. (Mirror)

Mshambuliaji wa Croatia Ante Rebic, 25, amejiunga na AC Milan kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili kutoka Eintracht Frankfurt, huku mshambulizi Andre Silva, 23, akitarajiwa kuchukua nafasi yake . (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Mshambuliaji Atletico Madrid Mcroatia Nikola Kalinic, 31, amaejiunga na Roma kwa mkopo wa msimu mzima huku klabu hiyo ya Serie A ikimtuma mshambuliaji wa Czech Patrik Schick, 23, kwa mkopo kwenda RB Leipzig. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Kiungo wa safu ya kati wa Mbrazil Rafinha Alcantara, 26, amesaini kandarasi ya kurefusha mkataba wake na Barcelona kabla ya kujiunga na Celta Vigo kwa mkopo utakaodumu msimu mzima. (Marca)

Mchezaji wa kiungo cha kati Mbelgiji Steven Defour, 31, ametia saini mkataba wa kujiunga na Royal Antwerp siku mbili baada ya kuafikiana na Burnley kuvunja mkataba wake. (Het Laatste Nieuws – in Dutch)

Winga wa Leicester Mualgeria Rachid Ghezzal, 27, amesema “nafurahi sana” kuwa katika nafasi ya kuhamia Fiorentina kwa mkopo. (Leicester Mercury)

Atalanta imemsaini beki Mholanzi Simon Kjaer, 30, kutoka Sevilla kuchukua nafasi ya mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel, ambaye mkataba wake ulivunjwa siku 24 baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Serie A. (Goal)

Winga Marcus Edwards,20, ambaye wakati mmoja alibatizwa jina la’Messi mdogo’ amehama Tottenham. (Sun)

Vilabu vya Ligi kuu ya Premia huenda vikaungana kushinikiza dirisha la uhamisho wa wachezaji msimu ujao uendane na ule wa Ulaya. (Telegraph)

Beki wa kusho wa Leeds Mbelgiji Laurens de Bock, 26, amesema kutazama filamu ya ‘Sunderland ‘Til I Die’ kulimsaidi katika kufanya uamuzi wa kujiunga na klabu hiyo ya League One. (Sun)

Imeandaliwa na BBC

SOMA NA HII  KOCHA HUYU ALIYEMNYOOSHA MBELGIJI WA YANGA ANAWINDWA ATUE JANGWANI