Home Uncategorized MILIONI 50 ZAZUA GUMZO YANGA

MILIONI 50 ZAZUA GUMZO YANGA


Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga bado haujawalipa fedha wachezaji wake ambazo ni shilingi milioni 50 za kitanzania.

Yanga waliahidiwa fedha hizo baada ya kuitupa nje Township Rollers katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mabao 2-1.

Taarifa zinaeleza kuwa wachezaji hao hawajajua mpaka sasa uongozi umekwama wapi juu ya fedha hizo walizoahidi.

Fedha hizo ziliahidiwa kuwa zitakuwa sehemu ya motisha kwa wachezaji hao ili wazidi kufanya vema katika michuano ya kimataifa.

Hivi sasa Yanga ipo katika maandalizi kuelekea mechi ya hatua ya kwanza dhidi ya Zesco United ya Zambia.

SOMA NA HII  MATOKEO YA MECHI ZA LEO, MABAO TANO YAKUSANYWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here