Home Uncategorized VITA YA MAGOLIKIPA WAWILI WA TIMU YA TAIFA YAPATA MBABE, KASEJA ANA...

VITA YA MAGOLIKIPA WAWILI WA TIMU YA TAIFA YAPATA MBABE, KASEJA ANA BALAA


VITA ya magolikipa wawili wa KMC ambao wote wanazitumikia timu zao za Taifa leo zimemalizka kwa mmoja kuibuka mbabe baada ya kuipeleka timu yake hatua ya makundi.

Juma Kaseja mlinda mlango wa Tanzania anayekipiga klabu ya KMC  na Jonathan Nahimana wa timu ya Taifa ya Burundi ambaye aliingia akichukua nafasi ya Justin Ndikumana dakika ya 119.

Kwenye mchezo wa leo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar baada Kaseja ameokoa penalti moja na mbili wapigaji wa Burundi wamekosa.

Kwa upande wa Tanzania mfunguzi alikuwa ni Erasto Nyoni kisha Himid Mao na msumari wa mwisho ukapachikwa na Gadiel Michael.

Tanzania inasonga mbele kwenye hatua ya makundi Kwa Ushindi wa penalti 3-0 baada ya dakika 120 kukamilika Kwa kufungana bao 1-1.

Ikumbukwe kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Burundi timu zote zilitoshana nguvu Kwa kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA YANGA ATUMIA DAKIKA 1,350 KUSAKA POINTI 26, MECHI MBILI ZA MWANZO ILIKUWA KICHAPO