Home Uncategorized AZAM FC YAJIONGEZEA NGUVU ZA KUIFUATA YANGA

AZAM FC YAJIONGEZEA NGUVU ZA KUIFUATA YANGA

IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa ushindi waliopata mbele ya Lipuli ni nguvu kwao kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga utakaochezwa Januari, 18 uwanja wa Uhuru.

Lipuli ilikubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa, jana Januari, 15.

Mabao ya ushindi kwa Azam FC yalifungwa na Idd Chilunda na Joseph Mahundi yalitosha kuipa pointi tatu timu ya Azam FC iliyo chini ya Kocha Arstica Cioaba.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 29 na kuwa nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 na Lipuli inabaki na pointi zake 25 ikiwa imecheza jumla ya mechi 17.

SOMA NA HII  KASEJA TUNAMSIFIA LAKINI TUKUMBUKE TULIPOMTENGA ILI TUSIRUDIE KWA WENGINE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here