Home Uncategorized KAGERA SUGAR: HAKUNA TIMU NINAYOIGOPA, NIKIFUNGWA NAFUNGWA KWELI, NIKIFUNGA NAFUNGA

KAGERA SUGAR: HAKUNA TIMU NINAYOIGOPA, NIKIFUNGWA NAFUNGWA KWELI, NIKIFUNGA NAFUNGA

MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa kilichompa ushindi mbele ya Yanga ni kujiamini na kuiruhusu timu yake icheze bila hofu.

Maxime aliingoza timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana, Januari 15 Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa hana hofu anapocheza na timu yoyote wakati wowote jambo linalomfanya kupata matokeo na mtego wake ukigundulika anachapwa.

“Kwenye wakati wa kucheza na timu yoyote ninawaruhusu wachezaji kucheza na sio kupaki basi ndio maana ikitokea ninashinda ninafunga kweli na nikibanwa ninafungwa kwa kuwa siruhusu kupaki basi,” amesema. 

Ushindi wa mabao 3-0 unaifanya Kagera Sugar kupata ushindi wake wa kwanza ndani ya mwaka 2020 kwani ilipoteza mechi zake zote mbili za mwanzo mwaka huu ilipocheza mbele ya Coastal Union na Polisi Tanzania ikiwa ugenini.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA YANGA UWANJA WA AZAM COMPLEX