Home Uncategorized LIVERPOOL YAGOMEA UBINGWA WA LIGI KUU ENGLAND

LIVERPOOL YAGOMEA UBINGWA WA LIGI KUU ENGLAND


KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa hawezi kujitangazia ubingwa kwa sasa kwa kuwa safari bado ngumu kuelekea kwenye ubingwa.

Liverpool wapo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 61 kibindoni baada ya kucheza mechi 22 huku mabingwa watetezi Manchester City wakiwa nafasi ya pili na pointi 48.

Klopp amesema: “Hapana, hapana, kwa sasa siwezi kusema kwamba nimeshafikia hatua ya kutwaa ubingwa sio kitu chepesi kutamka hata kama timu yangu inapata matokeo mazuri.

“Kikubwa ambacho ninakitazama ni kuona timu inashinda mambo mengine yatakuja baadaye kwani Ligi Kuu ya England sio kitu chepesi kwani bado mechi nyingi za kucheza lolote linaweza kutokea,” amesema.

SOMA NA HII  LUC EYMAEL AUCHAMBUA UBORA WA SIMBA...