Home Uncategorized MBELGIJI WA YANGA KUTESTI MITAMBO LEO MBELE YA KAGERA SUGAR, TAMBO ZATAWALA

MBELGIJI WA YANGA KUTESTI MITAMBO LEO MBELE YA KAGERA SUGAR, TAMBO ZATAWALA


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael na msaidizi wake Riedoh Berdien ambao wamepewa kandarasi ya mkataba wa mwaka mmoja na nusu leo watakuwa na mtihani wao wa kwanza kutesti mitambo yao mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Uhuru.
Kagera Sugar iliyo chini ya mzawa, Mecky Maxime mwaka 2020 ipo nafasi ya nane na imjikusanyia pointi 24 itakutana na Yanga iliyo nafasi ya saba na imejikusanyia pointi 25.
Yanga iliyokuwa chini ya Charlse Mkwasa imecheza mechi moja tu mwaka huu 2020 ilikuwa mbele ya Simba na ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 uwanja wa Taifa, huku Kagera Sugar ikiwa imecheza jumla mechi mbili na imepoteza pointi sita ilifungwa bao 1-0 na Coatal Union pia ilifungwa mabao 2-1 na Polisi Tanzania.
Luc amesema kuwa mpango wake mkubwa ni kuona timu inapata matokeo mazuri kwenye mechi zake zote atakazocheza ikiwa ni pamoja nah ii ya leo dhidi ya Kagera Sugar huku kwa upande wa Maxime amesema kuwa anawatambua Yanga lazima apambane kupata pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA YAPIGANA VIKUMBU KUPATA SAINI ZA MITAMBO HII YA MABAO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here