Home Uncategorized SIMBA YAIGEUKA BODI YA LIGI

SIMBA YAIGEUKA BODI YA LIGI


MBELGIJI Sven Vanderboeck ambaye ni kocha mkuu wa Simba, amelalamika kuwa wanatakiwa kujiandaa kwelikweli kutokana na ratiba yao kuwabana kwa sasa ambapo katika siku nane kutoka leo Jumatano watakuwa na mechi tatu za ligi ambazo ni ngumu kwao.

Jana Jumatano Sven aliendelea na kibarua chake kwa kucheza na Namungo FC ya Lindi, baada ya mechi hiyo Simba Februari Mosi, watacheza na Coastal Union kisha Februari 4, watacheza na Polisi Tanzania ambapo itakuwa mechi yao ya mwisho ya mzunguko wa kwanza.


Kocha huyo amesema kuwa wana mechi hizo tatu katika siku nane ambapo zitamnyima muda mwingi wa kukaa na wachezaji wake kwa ajili ya kufundishana na hata kutoa makosa ambayo watakuwa wanayafanya kwenye mechi zao.

“Katika siku nane zijazo tutakuwa na wakati mgumu kwa sababu tutalazimika tucheze mechi tatu bila ya kupumzika. Tutaanza kwa kucheza na Namungo (leo Jumatano), kisha Coastal Union na Polisi Tanzania. Mechi zote hizi kwetu ni ngumu lakini ni muhimu.

“Katika kipindi hicho tunaweza tukakosa muda mrefu wa kufundishana na wachezaji wangu na hata yale makosa ambayo tutakuwa tunayafanya uwanjani, likiwemo suala la kuruhusu mabao.

Lakini hakuna namna tutapambana kwa ajili ya kupata pointi,” alisema Sven. Simba wapo kileleni kwenye ligi wakiwa na pointi 41, baada ya kucheza michezo 16 ya ligi hiyo.
SOMA NA HII  YANGA YAMVUTIA KASI BEKI WA AS VITA