Home Uncategorized AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA NDANDA

AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA NDANDA


AZAM FC leo ina kibarua cha kumenyana na Ndanda FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba ilipoteza mchezo wake wa ligi kwa kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ambayo nayo jana ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Ruvu Shoting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ofisa Habari wa Azam FC Jaffary Maganga amesema kuwa kikosi kipo vizuri na wachezaji wana morali kubwa kutafuta ushindi.

“Mchezo wetu uliopita dhidi Coastal Union tulipoteza kwa sasa tunajipanga kupata matokeo mbele ya Ndanda, kikubwa ni sapoti ya mashabiki wachezaji watafanya kazi yao vizuri,”.

Mchezo huo uachezwa majira ya saa 10:00 jioni.

SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED WAMEAMUA KUINASA SAINI YA KINDA HUYU