Home Uncategorized BIASHARA UNITED KUMALIZANA NA JKT TANZANIA LEO

BIASHARA UNITED KUMALIZANA NA JKT TANZANIA LEO


FRANCIS Baraza, Kocha wa Biashara United amesema kuwa wachezaji wake wana morali kubwa na ana imani watasepa na pointi tatu mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Biashara United ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 31 itamenyana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 34 zote zimecheza mechi 22.

Baraza amesema:” Wachezaji wana morali  na ni matumaini yetu kuona kwamba tunapata pointi tatu mbele ya mpinzani wetu kikubwa mashabiki watupe sapoti,”.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA LEO KIMATAIFA