Home Uncategorized COASTAL UNION: HAIKUWA BAHATI YETU KUSHINDA MBELE YA YANGA, TUNAJIPANGA

COASTAL UNION: HAIKUWA BAHATI YETU KUSHINDA MBELE YA YANGA, TUNAJIPANGA

NAHODHA wa Coastal Union, Bakari Nondo amesema kuwa haikuwa bahati yao kuibuka na ushindi mbele ya Yanga jana Uwanja wa Mkwakwani Tanga licha ya kupambana kusaka pointi tatu.

Nondo mwenye bao moja na pasi moya alikuwa mhimihili wa timu wakati ikisaska ushindi mbele ya Yanga kipindi cha pili ilitengeneza nafasi nyingi ambazo hazikuleta matokeo na kufanya wagawane pointi mojamoja na Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe Nondo amesema:”Tulipambana ili kutafuta matokeo na bahati haikuwa yetu, kushindwa kushinda sio mwisho wa mapambano tutajipanga kwa ajili ya mechi zetu zinazofuata.

“Ushindani ni mkubwa kwani mchezo wetu uliopita dhidi ya Ruvu tulipoteza tukiwa hapa nyumbani jambo lililofanya tuongeze umakini,”.

SOMA NA HII  NAMUNGO:TUNAKIPIGA BILA SHIDA DAR ES SALAAM