Home Uncategorized COASTAL UNION V YANGA WAPIGANA MKWARA HUU

COASTAL UNION V YANGA WAPIGANA MKWARA HUU


JUMA Abdul, beki wa Yanga na nahodha msaidizi wa kikosi hicho amesema kuwa kesho watapambana mbele ya Coastal Union ili kupata ushindi mbele ya wapinzani wao utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Yanga itakaribishwa na Coastal Union iliyotoka kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-1 na Ruvu Shooting huku wao wakitoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa wachezaji wana morali kubwa na wamejipanga kupata matokeo mbele ya wapinzani wao Coastal Union.
“Ligi ina ushindani mkubwa nasi tunapambana kurejea kwenye ubora wetu, matumaini yetu ni kuona tunapata pointi tatu, mashabiki watupe sapoti kwani safu ya ulinzi makosa yetu tumeyafanyia kazi,” amesema Abdul mwenye pasi nne za mabao.
Bakari Mwamnyeto, beki na nahodha mwenye bao moja na asisti moja ndani ya Coastal Union amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kupata ushindi mbele ya wapinzani wao.
SOMA NA HII  ZAHERA ATAJA SABABU YA KUIPIGA CHINI MBAO MECHI YA KIRAFIKI