Home Uncategorized ERIC DIER KUCHIMBISHA SPURS ASIPOKUWA BORA

ERIC DIER KUCHIMBISHA SPURS ASIPOKUWA BORA


KOCHA Mkuu wa Tottenham Spurs, Jose Mourinho yupo kwenye mpango wa kutaka kumuuza kiungo mkabaji wake Eric Dier iwapo hatakuwa na msaada ndani ya timu hiyo.
Mkataba wa nyota huyo wa Spurs unameguka mwaka 2021 na mwenyekiti wa timu hiyo Daniel Levy anahitaji kumpata mchezaji mpya baada ya Christian Eriksen kusepa ndani ya timu hiyo.
Nyota huyo mwenye miaka 26 alisajiliwa kwa pauni milioni nne akitokea timu ya Sporting Lisbon.
Spurs ina mtihani mzito wa kumenyana na Astoon Villa ya Mbwana Samatta Februari 16 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi za timu zote mbili.

SOMA NA HII  NAMUNGO WALIA NA UWANJA GAIRO, MOROGORO