Home Uncategorized EYMAEL WA YANGA AMPA MAJUKUMU MAZITO MUIVORYCOAST

EYMAEL WA YANGA AMPA MAJUKUMU MAZITO MUIVORYCOAST


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amemtaka mshambuliaji wake Yikpe Gislein raia wa Ivory Coast kufunga mabao mengi.

Eymael amemtaka nyota huyo aongeze juhudi baada ya kutupia mabao mawili ndani ya Yanga.

Ametupia mbele ya Singida United wakati timu hiyo ikishinda mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi na alifunga bao la pili mbele ya Tanzania Prisons wakati timu yake ikishinda mabao 2-0 mchezo wa Kombe la Shirikisho.


“Yikpe anakaa kwenye eneo zuri na ana uwezo wa kufunga ndio maana amekuwa akifunga anapopata nafasi mimi nataka aongeze zaidi juhudi na afunge mabao mengi,” amesema.



SOMA NA HII  WATATU WATAJWA KURITHI MIKOBA YA SVEN SIMBA, MMOJA YUPO BONGO