Home Uncategorized ISHU YA WACHEZAJI YANGA KUTOLIPWA MKWANJA WAO YAFIKIA HAPA

ISHU YA WACHEZAJI YANGA KUTOLIPWA MKWANJA WAO YAFIKIA HAPA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unawalipa wachezaji wao mshahara wao kwa wakati pamoja na wafanyakazi wengine hakuna ambaye anwadai.

Taarifa ambayo imetolewa na Yanga imeeleza kuwa kumekuwa na habari zinazosambaa zikidai kwamba wachezaji wanadai mshahara jambo ambalo si la kweli.

“Mishahara yote ya wachezaji na wafanyakazi wa Klabu ya Yanga inalipwa na Klabu kupitia vyanzo vyake mbalimbali, hakuna mchezaji yoyote wa Yanga ambaye hajalipwa mshahara wake kwa sasa na kwamba wachezaji na wafanyakazi wote wa Yanga watalipwa mshahara wao wa mwezi wa pili kwa wakati,” imeeleza taarifa hiyo. 

SOMA NA HII  AZAM FC YAWEKA PEMBENI HISTORIA YA YANGA, YAZITAKA POINTI TATU