Home Uncategorized KAGERA SUGAR KUPOTEZEA MAUMIVU YA SIMBA KWA WABAYA WA SIMBA

KAGERA SUGAR KUPOTEZEA MAUMIVU YA SIMBA KWA WABAYA WA SIMBA


YUSUPH Mhilu, mshambuliaji namba moja ndani ya Kagera Sugar amesema kuwa wapo tayari kusepa na pointi tatu mbele ya JKT Tanzania mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kagera Sugar ilitoka kupoteza mbele ya Simba Uwanja wa Taifa kwa kufungwa bao 1-0 leo inakutana na JKT Tanzania walioitungua Simba kwenye mchezo wa pili wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Uhuru hivyo itafuta maumivu kwa wabaya wa Simba.

“Tupo sawa na maandalizi yamekamilika hivyo ni suala la muda tu kuona namna gani tutapata pointi tatu muhimu kwani mpira ni ushindani.

“Kwa nafasi ambayo ninacheza mimi ninachofikiria ni kufunga tu mabao hakuna kingine na mabao ndiyo yatakayotupa ushindi,” amesema.

Mhilu ametupia jumla ya mabao 9 akiwa ni miongoni mwa wazawa wenye mabao mengi ndani ya ligi na ametoa pasi mbili za mabao na timu yake imefunga mabao 30.

SOMA NA HII  YANGA WAONYESHENI GSM, WANASTAHILI KUBAKI JANGWANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here