Home Uncategorized KAGERA SUGAR: TUNAWAHESHIMU SIMBA ILA POINTI ZAO TUNAZITAKA PIA

KAGERA SUGAR: TUNAWAHESHIMU SIMBA ILA POINTI ZAO TUNAZITAKA PIA

UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa kesho utapambana Uwanja wa Taifa kupata pointi tatu mbele ya Simba.

Kagera Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime itakuwa na kibarua cha pili ugenini mbele ya Simba baada ya kile cha kwanza wakiwa wenyeji mzunguko wa kwanza kukamilika.

Maxime amesema kuwa:”Tumejiandaa kwa ajili ya mechi zetu zote za ligi, tunatambua wapinzani wetu uimara wao upo wapi nasi pia tunatambua kitu cha kufanya kitakachotupa matokeo.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna gani timu itapambana bila kujali ukubwa wa timu ambayo tunacheza nayo sisi tunawaheshimu wapinzani wetu,” amesema.

Kagera Sugar imeshinda mchezo wake uliopita mbele ya Mbao kwa kuifunga mabao 2-0 na Simba ilishinda mbele ya Lipuli kwa kufunga bao 1-0.

SOMA NA HII  SIMBA SIO KINYONGE ATUA BOTSWANA KIFALME