Home Uncategorized KMC YAKWAMA KUENDELEZA USHUJAA MBELE YA NAMUNGO ILIYOFUTA UTEJA WAKE

KMC YAKWAMA KUENDELEZA USHUJAA MBELE YA NAMUNGO ILIYOFUTA UTEJA WAKENAMUNGO FC iliyo chini ya Hitimana Thiery jana ilishinda mabao 2-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa na kufuta uteja mbele ya KMC.

Mabao yote mawili kwa upande wa Namungo yalifungwa na mshambuliaji wao Bigirimana Blaise aliyeanza kufunga dakika ya 12 na bao la pili alifunga dakika ya 84.

KMC ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa James Msuva dakika ya 84 na waliziacha pointi zote tatu Uwanja wa Majaliwa.

Kwenye mchezo wa kwanza waliokutana na Namungo KMC ilisepa na pointi tatu Uwanja wa Chamazi jana Namungo walifuta uteja jumla.

SOMA NA HII  NYONI AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA