Home Uncategorized KOCHA POLISI TANZANIA AFICHUA KILICHO NYUMA YA KUSHINDWA MBELE YA SIMBA

KOCHA POLISI TANZANIA AFICHUA KILICHO NYUMA YA KUSHINDWA MBELE YA SIMBA

MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa mchezo wake wa jana Februari,4 mbele ya Simba ulikuwa ni mzuri walichoshindwa ni uzoefu tu kupata pointi tatu mbele ya Simba.

Polisi Tanzania ilikubali kufungwa mabao 2-1 mbele ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Hamsini amesema kuwa wachezaji walionyesha uwezo wao wote na walijitahidi kupambana mbele ya wapinzani wao.

“Nawapa pongezi wachezaji wangu wameonyesha kile ambacho niliwaambia wafanye na walijitahidi kwa kweli. Kilichotushinda ni uzoefu tu kwani bado timu inajijenga taratibu na kuendelea kutafuta matokeo mazuri,” amesema.

Polisi Tanzania imecheza jumla ya mechi 19 imefikisha pointi 30 ipo nafasi ya saba kwenye msimamo.

Kwenye mchezo huo walianza kufunga bao la kwanza kupitia kwa Sisxtus Sabilo aliyekuwa msumbufu mwanzo mwisho dakika ya 22 na yale ya Simba yakifungwa na John Bocco dakika ya 56 na Ibrahim Ajibu dakika ya 90.

SOMA NA HII  SABABU ZA CHIRWA KUJIREJESHA AZAM ZAAINISHWA HADHARANI