Home Uncategorized MASHABIKI WAPEWA AHADI HII NA SIMBA LEO UWANJA WA TAIFA

MASHABIKI WAPEWA AHADI HII NA SIMBA LEO UWANJA WA TAIFA


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa leo watatoa soka safi kwa mashabiki wa Simba mbele ya Kagera Sugar.

Simba ina shuka Uwanja wa Taifa, Februari 18 ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 mbele ya Lipuli uliochezwa Februari 15 Uwanja wa Samora Iringa.

Sven amesema:”Wachezaji wapo vizuri na maadalizi yamekamilka kwa ajili ya mchezo wetu, tunaamini tutaoa soka safi kwa mashabiki wetu,”.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 56 baada ya kucheza mechi 22 za ligi na Kagera ipo nafasi ya sita na pointi zake 34.

SOMA NA HII  JAPO USHINDI NI MNONO ILA UKWELI WA LIGI KUU UPO HIVI