Home Uncategorized MEDDIE KAGERE AKWAMA DAKIKA 360 BILA KUTUPIA

MEDDIE KAGERE AKWAMA DAKIKA 360 BILA KUTUPIA


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amecheza mechi nne sawa na dakika 360 bila kufunga bao  kwenye Ligi Kuu Bara inayoendelea kwa sasa.

Kagere ambaye amehusika kwenye jumla ya mabao 17 kati ya 45 ya Simba akifunga mabao 12 na pasi tano za mwisho msimu uliopita alitupia jumla ya mabao 23.

Mara ya mwisho Kagere kufunga ilikuwa mbele ya Namungo alipofunga bao lake la 12 akimalizia pasi ya Sharaf Shiboub raia wa Sudan na Simba ilishinda mabao 3-2.

Hajafurukuta mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Taifa wakati Simba ikishinda mabao 2-0 na mfungaji wa mabao yote alikuwa ni Gerson Fraga.

Mbele ya Polisi Tanzania wakati Simba ikishinda mabao 2-1 Uwanja wa Taifa hakufuga, mbele ya JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru wakati Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru hakufunga.

Aliibukia Uwanja wa Jamhuri kwa kutoa pasi moja ya bao lililofungwa na John Bocco kwenye ushindi wa mabao 3-0 ila hakufunga.

Hivyo kwenye mechi nne Kagere hajafunga bao huku akiishia kutoa pasi moja ya bao. Kesho Simba itakuwa Iringa ikimenyana na Lipuli, Uwanja wa Samora, Iringa.
SOMA NA HII  KOCHA ZLATKO ATUA FIFA KISA KUFUTWA KAZI JUMLAJUMLA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here