Home Uncategorized MOLINGA APEWA ZIGO HILI NDANI YA YANGA

MOLINGA APEWA ZIGO HILI NDANI YA YANGA

DAVID Molinga, ‘Falcao’ amepewa mzigo mzito wa kufunga mabao mengi ndani ya Yanga na kujifunza kukaa kwenye nafasi akiwa ndani ya Uwanja.
Molinga ni kinara wa kutupia ndani ya Yanga, kwenye jumla ya mabao 24 waliyofunga Yanga yeye amefunga jumla ya mabao saba akifuatiwa na Patrick Sibomana mwenye mabao manne.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa amempa mbinu mpya mshambuliaji huyo zitakazomfanya aweze kuipa timu yake mabao mengi.
“Tuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji na ukitazama kinara wetu ni Molinga ana mabao saba hii ni idadi ndogo kwa timu inayotaka mafanikio, kikubwa ambacho nimemwambia awe anakaa eneo moja litakalomfanya afunge akitengenezewa nafasi.
“Kwa mechi ambazo amecheza taratibu nimeona kuna mabadiliko licha ya kwamba asili yake ya kuzungukazunguka ndani ya uwanja  huwa haikomi kwakwe,” amesema Eymael.
Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye ligi imejikusanyia pointi 39 kesho itamenyana na Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika, Moshi.
SOMA NA HII  AMBULACE YAZUA KIZAAZAA LIGI KUU BARA