Home Uncategorized MTIBWA SUGAR YAJIPA MATUMAINI KUTUSUA MBELE YA MBEYA CITY LEO

MTIBWA SUGAR YAJIPA MATUMAINI KUTUSUA MBELE YA MBEYA CITY LEO


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa baada ya kupata sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons leo ana imani ya kupata matokeo mbele ya Mbeya City.

Uwanja wa Sokoine leo Februari 22 utashuhudia vita ya kusaka pointi tatu kati ya Mbeya City na Mtibwa Sugar.

Katwila amesema:-“Tumekuwa tukishindwa kupata matokeo kutokana na ushindani uliopo kwenye ligi hilo kwetu halitupi shida kwani nasi tunaleta ushindani pia.

“Baada ya kupata sare mbele ya Prisons tumejifunza mbinu mpya na makosa yetu tumeyafanyia kazi tuna imani ya kupata matokeo mbele ya Mbeya City,”. 

SOMA NA HII  LACAZETTE AIBUA MASWALI KUPITA MITAA YA BARCELONA