Home Uncategorized PRISONS WAPANIA KULIPA KISASI KWA YANGA LEO TAIFA

PRISONS WAPANIA KULIPA KISASI KWA YANGA LEO TAIFA

ADOLF Rishard, Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, amesema kuwa leo watapambana mbele ya Yanga ili kulipa kisasi cha kuondolewa kwenye reli ndani ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Rishard alisema kuwa kikosi chake kilipoteza mwelekeo ndani ya ligi baada ya kufungwa na Yanga kwenye mchezo wao wa 13 jambo linalowafanya watafute namna ya kurejea kwenye ubora.
“Tulifungwa na Yanga mchezo wa kwanza Uwanja wa Samora, ukiachana na kwamba tulikuwa nje ya uwanja wetu tuliouzoea wa Sokoine, baada y kichapo kile tuliyumba, tumesahau yote tunajipanga kupata matokeo kwa sasa ili turejee kwenye ubora wetu,” amesema.
Bao pekee la ushindi kwa Yanga lilifungwa na Patrcik Sibomana mwenye mabao manne ndani ya ligi na ana pasi moja ya bao.
SOMA NA HII  MBAO FC YAINYOOSHA SIMBA MABAO 3-2 TAIFA DAR