Home Uncategorized SAUL APELEKA MSIBA LIVERPOOL, KLOPP AWAKARIBISHA ANFIELD

SAUL APELEKA MSIBA LIVERPOOL, KLOPP AWAKARIBISHA ANFIELD


SAUL Niquez nyota wa Atletico Madrid alipachika bao pekee la ushindi mbele ya Liverpool dakika ya nne kwenye hatua ya 16 bora ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliokamilika kwa Atletico kushinda bao 1-0.

Jitihada za Liverpool ambao ni Mabingwa watetezi ziligonga mwamba kwani wapinzani wao walikaza mwanzo mwisho na kujilinda.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Machi 11 Uwanja wa Anfield.

Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa mashabiki wa Atletico Madrid wajitokeze kwa wingi Anfield bila kukosa.

SOMA NA HII  YANGA HESABU ZAO SASA NI KUSEPA NA KOMBE LA LIGI KUU BARA