Home Uncategorized SIMBA WAELEZA JUU YA UJIO WA FLORENT IBENGE, BOSI AFUNGUKA

SIMBA WAELEZA JUU YA UJIO WA FLORENT IBENGE, BOSI AFUNGUKA


Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa ameweka bayana kwamba kocha wao mkuu, Sven Vanderboeck ataendelea kubakia katika nafasi yake japokuwa wamekuwa wakihusishwa na kumtaka raia wa DR Congo.

Senzo amesema kwamba wataendelea na kocha wao wa sasa katika nafasi hiyo huku wakimpa masharti ya kuwa timu hiyo kwa sasa haitakiwi kupoteza mechi yoyote.

Ibenge anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Sven ambaye inatajwa anaweza kutimuliwa kutokana na kutofanya vizuri kwenye timu hiyo. Senzo amesema kwamba suala la kumtaka Ibenge kwa sasa halipo licha ya kwamba mambo hayaendi vizuri kwa kocha wao.

“Unajua wakati ambao mambo yanakwenda vibaya ndipo kunaibuka mambo mengi. “Si kweli kwamba tunataka kocha mwingine kwa wakati huu.

Huyu aliyekuwepo anafaa lakini tunataka kuona timu haipotezi mechi kwa sababu hilo ni jambo la kuumiza kwa kila mmoja wetu hapa,” alisema Senzo raia wa Afrika
SOMA NA HII  JEMBE LA KAZI LA SIMBA LAIBUKIA KAGERA SUGAR