Home Uncategorized SIMBA YAGOMA KUPEWA SABABU ZA KUSHINDWA, YAZIPIGIA POINTI TATU ZA KAGERA

SIMBA YAGOMA KUPEWA SABABU ZA KUSHINDWA, YAZIPIGIA POINTI TATU ZA KAGERA


SIMBA kesho ina kazi mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Uongozi umesema kuwa hautaki sababu za kushindwa.

 Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime ina kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-0 na Simba mchezo wa kwanza liochezwa Uwanja wa Kaitaba.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa mpango mkubwa ni kupata pointi tatu mbele ya wapinzani wao kupitia wachezaji kujituma na ndani ya Uwanja.

“Kazi yetu ni kuona tunaendelea kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu tutakazocheza bila kuwa na sababu ya kujitetea,” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 56 baada ya kucheza mechi 22.

SOMA NA HII  AZAM FC YAKUBALI MUZIKI WA WANA KINO BOYS