Home Uncategorized SPURS SIO WATU WAZURI, WAIBAMIZA ASTON VILLA YA SAMATTA USIKU KWELI

SPURS SIO WATU WAZURI, WAIBAMIZA ASTON VILLA YA SAMATTA USIKU KWELI


ASTON Villa imekubali kichapo cha mabao 3-2 mbele ya Tottenham, kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa leo kwa kufungwa bao la usiku katika dakika za nyongeza.

Toby Alderweireld alichanganywa na Mbwana Samatta na kujifunga bao dakika ya 9 lilisawazishwa na yeye mwenyewe Toby dakika ya 27.

Kabla ya mapumziko Villa ilijichanganya na kufungwa bao la pili na Son Heung-min dakika ya 45+2 akimalizia penalti iliyopanguliwa na mlinda mlango wa Villa.

Mapumziko ilikuwa inaongoza Spurs kwa mabao 2-1 kipindi cha pili Bjorn Engels aliweka mzani sawa dakika ya 53 lilidumu mpaka dakika ya 90.

Hii inakuwa mechi ya pili kwa Mbwana Samatta kucheza ndani ya Ligi Kuu England baada ya kujiunga na Villa akitokea klabu ya Genk alianza.


Balaa lilipatikana dakika ya 90+4 kwa Son kutupia bao la tatu na la ushindi Kwa Spurs liliwamaliza nguvu Villa jumla.

Aston Villa ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi zake 25 na Spurs nafasi ya tano ikiwa na pointi 40 zote zimecheza mechi 26.

SOMA NA HII  DUH! KAMBI YA SIMBA SI YA MCHEZOMCHEZO