Home Uncategorized TFF YATOA SABABU YA KILICHOTIBUA LIGI KUU TANZANIA BARA

TFF YATOA SABABU YA KILICHOTIBUA LIGI KUU TANZANIA BARA


WILFRED Kidao, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa kilichotibua ratiba ya Ligi Kuu Bara kuwa kama ilivyo sasa ni kupanguliwa kwa ratiba ya michuano ya CHAN iliyotarajiwa kufanyika mwezi Januari.

Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa inaendelea huku timu zikicheza baada ya siku mbili kukimbizana na ratiba, Simba ilicheza Februari 15 na Lipuli leo inaingia kazini kumenyana na Kagera Sugar na Yanga pia ilikuwa kazini mbele ya Tanzania Prisons na leo itacheza na Polisi Tanzania iliyocheza na Azam FC Uwanja wa Uhuru.

 Kidao amesema :” Ratiba ya ligi ilitibuliwa na michuano ya CHAN awali tulitarajia ingefanyika mwezi Januari ila mwisho wa siku ikapangwa kufanyika mwezi Aprili, la licha ya kuwa hivyo tumelazimika kuifanya ratiba kwenda namna hii, kikubwa ni mpangilio mzuri na kuona namna gani tumu zitakwenda na kasi iliyopo kwani hatuna chaguo lingine,”.

Tanzania imepangwa Kundi D kwenye michuano ya CHN itakayofanyika nchini Cameroon, April 2020 ikiwa na timu za Guinea, Zambia na Namibia.

SOMA NA HII  GADIEL- WACHEZAJI WA SIMBA TUNA DENI