Home Uncategorized YANGA:POLISI TANZANIA WAGUMU ILA TUNAZITAKA POINTI TATU ZAO

YANGA:POLISI TANZANIA WAGUMU ILA TUNAZITAKA POINTI TATU ZAO


CHARLES Mkwasa, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Polisi Tanzania ni mgumu ila wamejipanga kupata pointi tatu muhimu.

Leo, Februari 18 Uwanja wa Ushirikia Yanga itakaribishwa na Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa majira ya saa 10:00.

Mkwasa amesema:”Polisi Tanzania ni timu imara ipo vizuri ukizingatia kwamba haijawa na mwenendo mbaya kwenye ligi, tunatambua mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga kufanya vema na kuona namna gani tutapata pointi tatu,”.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Yanga ililazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na ilishuhudiwa hat-trick ya kwanza kwa msimu wa 2019/20 ikifungwa na Ditram Nchimbi aliyekuwa Polisi Tanzania kwa sasa yupo Yanga.

SOMA NA HII  BREAKING:BEKI STARS ASAINI YANGA