Home Uncategorized MASHINDANO YA DIPLOMATIC GOLF MSIMU WA PILI KUANZA MEI 30

MASHINDANO YA DIPLOMATIC GOLF MSIMU WA PILI KUANZA MEI 30


MASHINDANO ya Diplomatic Golf msimu wa pili yanayoratibiwa na Kampuni ya Tanzania Mwandi kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, yanatarajiwa kuanza kuunguruma Mei 30, 2020 katika viwanja vya Kilimanjaro Golf Club, Usa River jijini Arusha.

Maandalizi ya mashindano hayo ambayo yanafanyika kila mwaka, yameendelae kwa nguvu leo Jumanne, Machi 17, 2020, katika Viwanja Gymkhana jijini Dar es Salaam.


Akizungumza viwanjani hapo wakati wa maandalizi hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema maadalizi hayo yanaendelea vizuri na kwa kiwango cha juu.


 “Maandalizi yanaendelea vizuri na tumefanikiwa kupata wadau wa ndani na nje ya nchi tutakaosaidiana nao kuendesha mashindano haya yenye lengo la kukuza wigo na kupanua mchezo wa golf nchini Tanzania.

 “Diplomatic Golf, ni fursa mahsusi kwa mawaziri, wabunge, wanasiasa, wanadiplomasia na wananchi wote wa kawaida kukutana na kubadilishana uzoefu wa mchezo huo na kutengeneza njia mbadala ya kuikuza tasnia hiyo kwa kushirikiana na wadau na wapenda golf, hivyo ninawasihi sote tujitokeze kwa wingi kushiriki mashindano haya,” amesema Ndumbaro.


Mwaka 2019, Mashindano ya Diplomatic Golf yalifanyika visiwani Zanzibar katika Viwanja vya Zanzibar Golf Course Sea Cliff, ambapo mwaka huu yanatarajiwa kuwa ya tofauti huku vitu vingi vikiwa vimeboreshwa zaidi.

SOMA NA HII  HUKU UNITED IKIMPIGA MTU 4-0, RASHFORD NA POGBA WACHEZAJI BORA WA MECHI