Home Uncategorized BAADA YA KUPATA CORONA, FA NA MENEJA WA DIAMOND WAWAONDOA WASIWASI WATANZANIA

BAADA YA KUPATA CORONA, FA NA MENEJA WA DIAMOND WAWAONDOA WASIWASI WATANZANIA


HAMIS Mwinjuma maarufu kama Mwana FA amesema kuwa licha ya kugundulika na Virisu vya Corona bado yupo fiti asilimia mia.

FA  amethibitisha kuwa amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona na sasa yupo chini ya uangalizi na afya yake inaendelea vizuri.

“Nipo sawa asilimia mia, na nimejitenga tangu niliporudi sijakutana na familia yangu ninawaomba tuchukue tahadhari kwani sisi tulioandamwa  na migonjwa mikubwa katika kukua kwetu haya ‘mafua’ wala siyo kitu cha kututisha, tuweni na amani mioyoni mwetu,” amesema.

Pia mwingine ambaye amethibitisha kukutwa na Virusi vya Corona ni Meneja wa Nasib Abdul ‘ Diamond’ Sallam Ahmed Sharaff ‘Sallam SK’ naye amesema kuwa anaendelea salama.

Aidha wote wameishukuru Serikali kwa huduma nzuri wanayopata na wamewasihi Watanzania kufuata ushauri wa Wizara ya afya.

SOMA NA HII  LIGI DARAJA LA KWANZA TUSIIFUMBIE MACHO KWANI HUKU MAMBO BADO