Home Uncategorized DITRAM NCHIMBI: NINAFANYA MAZOEZI KULINDA KIWANGO CHANGU

DITRAM NCHIMBI: NINAFANYA MAZOEZI KULINDA KIWANGO CHANGU


DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa licha ya kuwa kwenye mapumziko bado anaendelea kufanya mazoezi ili kuwinda kiwango chake.

Nyota huyo mwenye mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara alifunga mabao mawili akiwa na Yanga na manne alipokuwa Polisi Tanzania kabla ya kujiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nchimbi amesema kuwa kwa muda huu wa mapumziko baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa anaendelea na mazoezi ili kulinda kiwango chake.

“Ni wakati wa kuomba na kuona namna gani tutapita salama katika kipindi hiki kigumu cha maambukizi ya Virusi vya Corona, kutokana na ligi kusimama nimekuwa nikiendela na mazoezi binafsi ili kulinda kiwango changu.

“Ninachukua tahadhari mimi binafsi pamoja na familia kiujumla ambapo tumekuwa tukizingatia yale yanayohusu usalama wetu pamoja na wengine, kikubwa ni kuomba ili kila kitu kiwe sawa,” amesema.

Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali ya Tanzania, Machi 17 na inatarajiwa kurejea Aprili 17 iwapo hali ya maambukizi ya virusi vya Corona yatapungua.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ACHARUKA, AMTAJA AKAPOMBE - VIDEO