Home Uncategorized HAWA JAMAA WANABALAA LA KUCHEKA NA NYAVU

HAWA JAMAA WANABALAA LA KUCHEKA NA NYAVU


HAWA hapa wakali wa kucheka na nyavu msimu huu wa 2019/20 kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara namna hii:–

Meddie Kagere, mshambuliaji wa Simba ni kinara wa kucheka na nyavu anaendelea pale alipoishia msimu uliopita ambapo alikuwa ni kinara kwa kutupia mabao 23, msimu huu ametupia mabao 19.

Yusuph Mhilu, nyota huyu mzawa wa Kagera Sugar aetupia mabao 11 na miongoni mwa timu alizozipa tabu ni mabosi wake wa zamani Yanga wakati ikishinda kwa mabao 3-0 Uwanja wa Uhuru. 


Reliants Lusajo, jamaa analijua lango na ni msumbufu akiwa ndani ya Uwanja, anakipiga Namungo na aliwahi kucheza pia Yanga ila hakupata nafasi ya kuwika kibindoni naye ana mabao 11.

Paul Nonga, ni nahodha wa Lipuli ambayo kwa sasa mwendo wake ni wa kusuasua tofauti na ilivyoanza mwanzo ligi, ametupia mabao 11 na pasi nne za mabao.

Bigirimana Blaise, raia huyu wa Rwanda amezitungua timu zote zenye maskani yake pale Msimbazi alianza kuitungua Simba akamalizia na Yanga, kibindoni ana mabao 10.


Peter Mapunda, shujaa wa Mbeya anakipiga ndani ya Mbeya City ana balaa akiwa ndani ya Uwanja mguuni ana mabao 9.


Daruwesh Saliboko pacha yake na Nonga ni balaa pale Lipuli yeye ametupia mabao nane kama ilivyo kwa David Molinga wa Yanga, Ayoub Lyanga wa Coastal Union na Obrey Chirwa wa Azam FC.

SOMA NA HII  NYOTA HAWA WATANO SIMBA KUIKOSA IHEFU FC LEO