Home Uncategorized ILANFYA WA KMC AIMALIZA JUMLAJUMLA ALLIANCE UHURU LEO

ILANFYA WA KMC AIMALIZA JUMLAJUMLA ALLIANCE UHURU LEO

CHARLES Ilanfya, mshambuliaji wa KMC leo ameifungia timu yake mabao mawili na kuipa pointi tatu timu yake wakati ikishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Alliance FC,

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara umechezwa leo, Machi 15 Uwanja wa Uhuru.

Kipindi cha kwanza Ilanfya aliandika bao la kwanza dakika ya 44 na kipindi cha pili alifunga bao dakika ya 80 huku lile la Alliance likifungwa na Michael Chinedu dakika ya 90+5.

Ushindi huo unaifanya KMC kuwa nafasi ya 15 kwenye msimamo ikiwa na pointi 33 huku Alliance FC ikiwa nafasi ya 18 ikiwa na pointi 29 zote zimecheza mechi 29.

SOMA NA HII  YANGA SASA WAWATAMANI AL AHLY BAADA YA SIMBA KUSHINDWA KUTAMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here