Home Uncategorized JURGEN KLOPP AIPA TANO WATFORD KWA KUMTIBULIA REKODI YAKE MAZIMA

JURGEN KLOPP AIPA TANO WATFORD KWA KUMTIBULIA REKODI YAKE MAZIMA


KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa wapinzani wao Watford walistahili kushinda mabao 3-0 waliyoyapata kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England.

Mchezo huo uliochezwa uwanja Vicarage Road ulikuwa ni wa kwanza kwa Liverpool kupoteza kwenye ligi msimu huu baada ya kucheza siku 422 bila kufungwa.

Mabao ya Watford yalifungwa na Ismaila Sarr aliyefunga mawili dakika ya 54 kabla ya kuongeza msumari mwingine dakika ya 60 na msumari wa mwisho na wa tatu ulipachikwa na Troy Deeney dakika ya 72 na kuifanya Liverpool kupoteana.

Klopp amesema kuwa kufungwa mabao 3-0 ugenini inamaanisha kwamba walizidiwa na wapinzani wao wanastahili pongezi kwa kuwa wamefanya kazi kubwa na ngumu kushinda.

SOMA NA HII  SPURS YAHAHA KUMBAKIZA KANE NDANI YA KIKOSI