Home Uncategorized MVUA YATIBUA MAMBO HUKO IRINGA MPAKA SHINYANGA, SALAMU ZIPO NAMNA HII

MVUA YATIBUA MAMBO HUKO IRINGA MPAKA SHINYANGA, SALAMU ZIPO NAMNA HII


Mechi ya Ligi Kuu Bara leo Kati ya Lipuli na Ndanda FC imeahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha mkoani Iringa hali iliyosababishwa sehemu ya kuchezea Uwanja wa Samora kujaa maji.

Pia mchezo kati ya KMC v JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru, Mwadui FC na Polisi Tanzania Uwanja wa Kambarage yote imeahirishwa kutokana na mvua.


Pia kutokana na hofu ya ugonjwa wa Corona wachezaji wameambiwa na Shirikisho la Soka la Mpira Tanzania (TFF) kutopeana mikono na badala yake watatumia njia mbadala.

SOMA NA HII  CHAMA CLATOUS AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA YANGA