Home Uncategorized NAMUNGO YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA

NAMUNGO YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kinajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Jumapili Uwanja wa Majaliwa.

Namungo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 49 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya tatu na pointi 50 kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini wanakutana na timu bora jambo linalowafanya nao wajiweke sawa kusaka pointi tatu.

“Tutakuwa nyumbani na tunatambua kwamba mchezo wetu utakuwa na ushindani hilo lipo wazi, tumejipanga na matumaini yetu ni kuona tunapata pointi tatu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.

Mchezo huu unakuwa wa kwanza kwa Yanga kukutana na Namungo msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara baada ya Namungo  kupanda Daraja msimu wa 2019/20. 

SOMA NA HII  MABOSI WA YANGA HUENDA 'WANAUMA MENO' DILI LA DICKSON JOB KWA UWEZO WA NINJA