Home Uncategorized NGULI WA UNITED ATAJA KINACHOMBEBA BRUNO FERNANDES

NGULI WA UNITED ATAJA KINACHOMBEBA BRUNO FERNANDES


BRUNO Fernandes, nyota wa Manchester United amekuwa msaada mkubwa ndani ya Klabu hiyo kwa sasa.

Nguli wa zamani wa Klabu ya Manchester United Bryan Robson amepongeza uwezo wa nyota huyo huku akitaja sababu inayombeba mshambuliaji huyo.


 “Nafikiri kinachosaidia ni kuwa alikuwa nahodha wa Sporting uongozi ni kitu ambacho unakuwa nacho pia kipaji alichonacho kinambeba. 

“Anaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, kushambulia, kufunga na kutengeneza mashambulizi anapenda kazi yake na anapenda kuona wenzake wakiiga kile anachofanya,” amesema.

Fernandes amefunga mabao matatu na kutoa pasi nne akicheza mechi tisa ndani ya United.

SOMA NA HII  HUO MKATAB WA AZIZ KI NI KUFURU