Home Uncategorized NJIA RAHISI YA KUPATA NDINGA MPYA KWA BEI CHEE IPO HIVI

NJIA RAHISI YA KUPATA NDINGA MPYA KWA BEI CHEE IPO HIVI


SIYO hadithi tena za kale, kwani ukiwa mjanja kwa kusoma magazeti ya Championi au Spoti Xtra kila wiki, unaweza ukawa miongoni mwa watu ambao wanaweza wakalala masikini na kuamka matajiri.

Huu siyo mchezo wa kubeti, hii ni bahati nasibu ambayo Championi na Spoti Xtra wameamua kumtunuku mtu wake mmoja wa nguvu, katika karne hii ya 21.

Ona, yaani unanunua gazeti la Championi kwa shilingi 800 au Spoti Xtra kwa tsh 500, unapata habari kali za Bongo za michezo na burudani, unapata makala tamu za ndani na Ulaya, halafu kama hiyo haitoshi, mwisho wa picha unaondoka na Toyota FunCargo mpya, unaenda kuwatambia mtaani kwenu.

Pengine haujanielewa, Ishu inayokimbiza kwa sasa katika mitaa mingi ya nchi hii, ni bahati nasibu iliyoanzishwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra.

Bahati Nasibu hiyo iliyopewa jina la Chomoka na Gari Mpya, inawahusu wasomaji wote wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra, ambayo yanazalishwa na Kampuni Mama ya Global Publishers.

Lakini mbali na mshindi wa jumla kuchomoka na ndinga, wapo ambao kila wiki watakuwa wanajidai na simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio.

Timu ya masoko ya Championi na Spoti Xtra, ikiongozwa na Anthony Adam, imekuwa ikizunguka katika mitaa mbalimbali ya Tanzania, ikiwa inatoa elimu kwa watanzania ambao bado hawajapata uelewa mzuri juu ya bahati nasibu hiyo.

Leo Alhamisi, timu hiyo iliendelea na ziara yetu ya kulizunguka jiji la Dar es salaam, katika mitaa ya Mabibo, Vingungunguti, Tabata na Buguruni na kuendelea kuwahamasisha watu kuendelea kusoma magazeti ya Championi na Spoti Xtra na kushiriki bahati nasibu hiyo.

Akizungumza na https://ift.tt/1GYNUKV, Mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Global Publishers, Anthony Adam amesema; “Katika kila mtaa tuliopita tuligawa zawadi za bure kwa watu wote ambao walikutwa na gazeti la Spoti Xtra, tulichezesha droo kwa washiriki wote na walijinyakulia zawadi za papo kwa papo. 


“Kwa wale wa mikoani, zamu yao ya mtaa kwa mtaa inakuja, ambapo wiki ijayo tutaanza na mkoa wa Mwanza.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA HUU HAPA